Wanafunzi wa
Kitanzania Urusi
wavamia ubalozini
na Deogratius Temba
WANAFUNZI wa Kitanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Lumumba nchini Urusi, wamepiga kambi katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini humo, kwa madai ya kutaka kulipwa posho zao za kujikimu.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Urafiki Cha Urusi mjini Moscowwakiwa kwenye sherehe mojawapo zilizofanyika chuoni hapo. Hao
ni wanafunzi kutoka Benin na Madagaska.
Picha Chama Cha Watanzania Oslo.
Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka Urusi zinasema wanafunzi hao wameweka kambi ubalozini hapo kwa siku mbili mfululizo kuanzia juzi, bila kupata chakula, wakishinikiza walipwe posho zao.
Kutokana na hali hiyo, inadaiwa kuwa polisi nchini humo nao wameweka ulinzi mkali katika ofisi hiyo, huku juhudi za kuwataka wanafunzi hao waondoke zikiendelea bila mafanikio. Jitihada za kuwataka waondoke zimekuwa zikiendelea kwa muda wa siku mbili sasa bila mafanikio.
Bofya na endelea>>>>>
Hicho chuo sasa kinaitwa:
Peoples' Friendship University of Russia
Baadhi ya watu mashuhuri waliosoma chuo hicho ni:
1. Ilyich Ramirez Sanchez - Carlos the Jackal. Gaidi maarufu la kimataifa
2. Mohammed Boudia - alikuwa anafanana na Carlos naye alikuwa gaidi na mshiriki wa Carlos, aliuawa na Mossad mjini Paris. Mossad walidhani wamemwua Carlos.
3. Mahmoud Abbas (a.k.a Abu Mazen), Rais wa Wapalestina
4. Mustafa Barghouti
5. Lucy Seki

No comments:
Post a Comment