Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo
Mpenzi Frank,
Vipi huko? Najua maisha yanazidi kuwa magumu na bila shaka sasa watembea zaidi kutokana na nauli hizi. Pole sana mpenzi wangu. Lakini bila shaka sasa umekuwa fiti kwelikweli. Kutembea kote huko!
Basi na hapa wiki hii imekuwa vurumai kwelikweli. Juzijuzi bosi katoka kwenye madhifa yao (sielewi kwa nini wanapenda kula nchi waziwazi kiasi hicho! Pamoja na kuiba pesa zote sasa wanataka kusababisha uhaba wa chakula pia!) Basi bosi karudi. Kama kawaida nilitakiwa kuamka na kumfungulia mlango hivyo niliwahi pale mlangoni niliposikia gari linaingia. Nikafungua mlango na kusubiri. Ghafla nikasikia Paaaaaaa! Niliogopa mpenzi, nilifikiri tunavamiwa. Nikafunga mlango harakaharaka lakini nikasikia sauti ya bosi likimwamrisha mlinzi.

No comments:
Post a Comment