CCM mchezo
wa kuigiza?
Na Simon Mhina
Maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kumteua Andrew Chenge, kuwa mmoja wa wajumbe wa Timu ya watu watatu ya kupitia mkataba wa jengo jipya la Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), umezua taharuki kubwa na watu wanahoji busara ya kumteua mtu mwenye tuhuma nyingi kufanya kazi hiyo.
Watu wa kada mbalimbali wakitoa maoni yao siku moja tu baada ya uteuzi huo, wamedai kuwa Chenge maarufu kwa jina la `mzee wa vijisenti` ana tuhuma ambazo zinachunguzwa na vyombo vya ndani na nje ya nchi.
Chenge anachunguzwa na taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (Serious Fraud Office SFO) kwa madai ya kuhusikika na tuhuma za rushwa katika ununuzi wa rada.

No comments:
Post a Comment