JK aungwe mkono,
wananchi wasipuuzwe
katika kukomesha
vitendo vya ufisadi
Yamewahi kujitokeza maneno mengi maarufu nchini katika miaka ya karibuni lakini sidhani kama yamewahi kujitokeza maneno yanayotumika sana katika jamii ya Kitanzania kama maneno Richmond, fisadi, au EPA.
Sijawahi kufanya utafiti kufahamu ni kwa nini imekuwa hivyo lakini nina uhakika kuwa watu wa kada zote wanayatumia hasa katika mazungumzo ya kawaida yanayohusu fedha, utajiri, wizi na mengine yanayohusiana na hayo.
Imekuwa hivyo si kwa bahati mbaya, msingi wa umaarufu wa maneno hayo ni fedha, Richmond ulikuwa Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) na kampuni hewa ya Richmond iliyopaswa kuzalisha nishati hiyo ili iingizwe katika gridi ya Taifa kupunguza ukubwa wa tatizo la umeme wakati huo.
No comments:
Post a Comment