CCM inahitaji ujasiri
wa ANC kumweka
sawa JK
WIKI iliyopita, ilimalizika kwa matukio mazito mawili ya kisiasa ambayo yote yalimgusa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, ambaye kesho anahitimisha kipindi chake cha urais kilichokatishwa.
Tukio la kwanza lililomgusa kiongozi huyo wa moja ya mataifa makubwa ya Afrika likiwa na nguvu ya kiuchumi, ni lile la kuhitimishwa kwa mazungumzo magumu ya kutafuta suluhu ya kisiasa katika nchi ya Zimbabwe, Mbeki aliyasimamia na kuyaongoza katika mazingira ambayo kimsingi yalikuwa magumu na yenye mabonde na milima.
Watu wanaofuatilia siasa za Zimbabwe ni mashahidi wazuri wa namna Mbeki alivyoweza kuhimili vishindo vya upinzani ama kutoka kwa Rais Robert Mugabe au mpinzani wake, Morgan Tsvangirai, kwa nyakati tofauti.
No comments:
Post a Comment