Thursday, September 11, 2008


Kwani nchi hii

inatawaliwa kijeshi?


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo


Mpenzi Frank,

VIPI hali yako mpenzi?  Ni matumaini yangu kwamba wewe ni mzima kuliko mimi maana nasumbuliwa na malaria vibaya sana.  Nilitaka kwenda hospitali mapema nilipohisi hali imebadilika lakini mama Bosi alisema kwanza nimalize kazi. 

Nilipojaribu kumwambia kwamba hali yangu kweli ni mbaya alianza kufoka.

‘We Hidaya, nilikuamini sana.  Sasa waanza kutega kazi namna hii?  Itakuwaje wakija wageni na kukuta nyumba chafu?’

Bofya na endelea>>>>>


No comments: