Thursday, September 25, 2008

Mbele ya njaa

uvumilivu upo kweli?



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.



Mpenzi Frank,

wacha kukasirika baba.  Wewe unasahau kuniandikia mara nyingi lakini mimi nikitumia kaofu kangu kumwandikia shoga yangu aliyepotewa na mtoto wawaka moto kama kifuu cha nazi.  Vibaya hivyo mpenzi!  Tena nilikuandikia kinoti kukuelezea kwa nini imekuwa hivyo. 

Hata hivyo, nimefurahi sana kupata kaofu kingine nikuandikie tena.  Mara nyingine natamani kugoma kama hawa wafanyakazi wa benki.  Hivi kwa nini wanene hawashtuki hadi wembamba wawabambe na mgomo.  Yaani wafanyakazi wakitumia njia za ustaaarabu kuomba, kueleza, wanadanganywa na maneno matamumatamu na ahadi duni na baada ya hapo hakuna linalotokea.  Wakijaribu kushinikiza kidogo, wanatishwa .. mpaka wafanye kweli.  Hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa?  Hii serikali yetu inayodai inapenda sana haki, haki na haki tena, mbona haitendi haki mpaka ishinikizwe hivyo?  Bofya na endelea>>>>>


No comments: