MUSENDO:
Nilishuhudia mfungwa
akiuawa gerezani
kwa kipigo
Zephania Musendo ni mwanahabari ambaye hivi karibuni ametoka gerezani baada ya kumaliza kifungo cha miaka mitano kutokana na kukutwa na hatia ya kuomba na kupokea rushwa.Makala hii ya Mwandishi John Ngunge yazungumzia mtazamo wake wa maisha.
Anaonekana kuwa na uso wa furaha. Bila shaka yo yote furaha yake inatokana na kumaliza kifungo chake jela cha miaka mitatu na nusu.
Huyo ni Zephania Musendo, ambaye alikuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Family Mirror kabla ya Mahakama ya Kisutu kumhukumu kwenda jela miaka mitano kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa.
Hukumu hiyo ilitolewa Mei 17, 2005 baada ya kutiwa hatiani.Katika shitaka lilimtia hatiani ilisemwa kuwa alimuomba rushwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea. Wakati huo alikuwa mmoja wa wakurugenzi katika Taasisi hiyo.

No comments:
Post a Comment