Tuesday, September 02, 2008



wafichua siri



HATIMAYE siri ya kuvunjwa kwa maandamano ya kupongeza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa bungeni hivi karibuni imejulikana, baada ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kubaini kuwapo kwa wanachama wao waliopanga kuja na mabango ya kupinga hotuba hiyo wakati lengo likiwa kupongeza.

Maandamano hayo yalipangwa kufanyika Jumapili iliyopita na kupangwa kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Saleh Ramadhan Ferouz, lakini yaliahirishwa kutokana na sababu hizo na kusababisha mtafaruku mkubwa ndani ya chama visiwani, Zanzibar.

Akizungumza na Tanzania Daima, Khamis Haji, ambaye ni kada wa CCM, alisema baadhi ya wanachama wa chama hicho Zanzibar, wanapinga hotuba ya Rais Kikwete na kama maandamano hayo yangefanyika, yasingepata watu ama yangekuwa na wafuasi wao wanaopinga.





No comments: