OIC:
JK, Membe,
mtushinde kwa
hoja si kwa vioja
SABABU kubwa inayotolewa na wale wanaotaka Tanzania ijiunge na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ni kuwa tukifanya hivyo Tanzania itapata misaada inayohitajika.
Aliyesema vizuri kuhusu mawazo ya namna hii ni Mufti Msaidizi Sheikh Suleiman Gorogosi, ambaye akizungumza na gazeti mojawapo la Kiswahili siku chache zilizopita alisema kuwa “Hili hatulikubali. Serikali imeshasema OIC haina madhara, lazima tujiunge, tena mpango wa kuiingiza nchi ndani ya OIC uharakishwe ili watu tupate maendeleo.”
Katika makala zangu mbili zilizotangulia kuhusu suala hili ukiondoa majibu ya watu wenye kebehi na ambao hawana hoja wamebakia kudai kuwa Tanzania ikijiunga na OIC basi tutapata misaada mingi ambayo itatulea maendeleo. Hivyo, sisi wengine tunapopinga kulazimishwa kwa Tanzania kujiunga basi tunaonekana kana kwamba tunazuia misaada na hivyo tunazuia maendeleo.
No comments:
Post a Comment