Tanzania isilazimishwe
kujiunga na OIC - 2
na Mwanakijiji
KUNA watu ambao kwa makosa yao wanaamini kwamba mtu akihoji jumuiya ya Kiislamu, hoja za Waislamu au mipango ya Waislamu inayohusisha maslahi hata ya wasio Waislamu au ya nchi nzima, huyo ni mdini, ana chuki na hawatakii mema Waislamu.
Watu hawa hawaangalii hoja, maelezo au kina cha maneno yanayozungumzwa katika mjadala fulani, wanachoangalia ni kama mtu anawaunga mkono au anawapinga na wakigundua anawapinga badala ya kuangalia hoja, wanakimbilia kutoa madai ya chuki dhidi ya mtu huyo.
No comments:
Post a Comment