Tuesday, September 23, 2008

Windows 7 Badala ya Vista?



Kwa wanaofuatilia maendeleo ya haraka ya TEKNOHAMA, Microsoft wako mbioni kutoa toleo la majaribio, Windows 7 (beta version) hivi karibuni. Inasemekana kuwa, hili la toleo la majaribio litakuwa kwenye ajenda ya "Professional Developers Conference" mwishoni mwa mwezi Oktoba. Vile vile hili lipo kwenye "Hardware Engineering Conference (WinHEC)" utakaofanyika mwanzoni mwa Novemba. Wachunguzi wa TEKNOHAMA wanadai kuwa toleo rasmi la Windows 7 litatolewa mwishoni mwa mwaka 2009 au mwanzoni mwa 2010.


No comments: