Tuesday, October 21, 2008



Albino mwingine

auawa



Raymond Mihayo, Kahama, Jumatatu 20. Oktoba

Binti albino aliyekuwa akisoma darasa la tatu wilayani humu ameuawa na watu ambao walinyofoa sehemu za nyama za mgongoni na kukata mkono wake mmoja. Mamia ya wakazi wa Kijiji cha Shilela Kata ya Segese wilayani humu walimiminika kwa wingi jana kushuhudia maziko ya binti huyo, Esther Charles, ambaye aliuawa usiku wa kuamkia Jumapili. 

Diwani wa Kata ya Segese, Joseph Manyara, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku katika familia ya Mtendaji wa Kijiji, Mzolewa Mashili. Alisema kuwa watu hao waliingia katika nyumba hiyo kwa kubomoa mlango wakitumia jiwe maarufu la 'fatuma'. 

Alisema baada ya kubomoa mlango huo na kuingia ndani walimkuta mama wa mtoto huyo, Jane John, akiwa naye lakini wakamnyang’anya na kumchukua hadi bafuni walikomuua. 

Kwa mujibu wa Diwani huyo, watu hao wasiojulikana waliviosha kwa maji viungo vya mtoto hapo hapo nyumbani pengine kwa lengo kuwa damu isimiminike kwa wingi wanapoondoka. Watu waliotoka vijiji mbalimbali kuhudhuria maziko ya Esther walisema kuwa mauaji hayo ni ya kinyama na hayajawahi kutokea katika kijiji hicho na Kata nzima ya Segese. 

Mauaji ya Esther yametokea siku ambayo kulifanyika maandamano mjini Dar es Salaam ya maalbino kupinga mauaji wanayofanyiwa. Maandamano hayo yalipokewa na Rais Jakaya Kikwete 


No comments: