Itakuwaje wakisikiliza
watoto na vijana na
kuwafanya washiriki
badala ya walengwa
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
VIPI mpenzi wangu, naona kazi imekubana kabisa. Yaani unakuja hapa Dar lakini wapata nafasi ya kuniona dakika 10 tu. Pole sana ya kazi!
Nilifurahi sana kukuona pia, angalau usuuze roho yangu kidogo lakini jamani dakika 10 tu. Umeniacha na misononeko mizito sana moyoni. Lakini Ulirudi salama juu ya lori lile. Utadhani wewe mwalimu anayekuja kudai haki zake!
Upande wangu mimi mzima ila naona siku hizi Mama Bosi na Binti Bosi wanapokezana kugombana na bosi mwenyewe, hadi bosi anaenda kulala mapema ajiepushe nao. Safari hii BB alikuja juu kwa nini watoto hawapati nafasi ya kushiriki.
No comments:
Post a Comment