Thursday, October 16, 2008


Jamaa mmoja alitia fora katika hoteli moja ya kifahari ambapo alifika na kukuta Menyu ikisomeka, Kuku mzima 3000/= Jamaa alipoona vile fasta aliagiza ili aweze kujipoza, baada ya muda aliletewa huyo kuku aliyeagiza na mambo yakawa hivi.
Jamaa: Huyu ndiye kuku mzima?
Mhudumu: Ndiyo!
Jamaa: Shenzi taipu! Hivi unaweza kunitapeli mimi nimekuagiza kuku mzma mbona kichwa sikioni, utumbo je? Yaani hata miguu na shingo yake havipo....! utalipa mwenyewe. Wateja wote wakabaki mdomo wazi, jamaa huyoo!...


No comments: