Hata tumbili hung'amuka

JUZI tuliadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Mwalimu Julius Nyerere miaka tisa iliyopita. Hakika, siku hii sasa imekuwa muhimu sana. Watanzania wanamkumbuka Mwalimu.
Baba wa Taifa alisimama upande wa wanyonge katika kila alilotenda. Alidhamiria kuwakomboa Watanzania kifikra ili waondokane na unyonge na umasikini wao. Hakika alikuwa kiongozi wa kanuni, kilichokufa ni kiwiliwili, Nyerere na fikra zake vi hai katika mioyo ya Watanzania wengi.
No comments:
Post a Comment