Jinamizi la OIC:
Maaskofu wambana
*64 wasaini waraka kumtaka ajiuzulu
*Watishia kubadili msimamo kwa CCM
*Wahoji zigo la ufisadi EPA jepesi?
*Waziri ajibu: Msinikariri vibaya
Na Gaudence Massati
MAASKOFU wa Jumuiya ya Wakristo Tanzania (CCT), wamemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, ajiuzulu ili apate wigo mpana wa kufanyia kazi walichokiita 'hamasa za kidini' alizonazo.
Pia CCT imeitahadharisha CCM, kuwa ingawa haifungamani na chama chochote cha siasa, lakini kwa kutokuwa makini na suala la Mahakama ya Kadhi na Tanzania kujiunga Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC), itabidi jumuiya hiyo ifikirie upya mtazamo wake kwa chama hicho kwa manufaa ya Watanzania......bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment