‘Taifa liko hatarini’
WANASIASA, viongozi wa dini na wananchi wameelezea kushitushwa kwao na hali ya kisiasa na kiuchumi inavyoendelea nchini, wakisema kwa sasa nchi iko hatarini kutokana na kuibuka kwa matabaka ya wazi ya kijamii miongoni mwa wananchi, watawala na watu waliowazunguka.
Matukio ya hivi karibuni kuhusiana na migomo, maandamano, ‘zomea-zomea’ na hata urushaji wa mawe dhidi ya msafara wa Rais wa Jamhuri, yameelezewa kuwa ni dalili za wazi za kuwapo ombwe la kisiasa na hatua nyingine katika mmomonyoko mkubwa wa maadili na kutoweka kwa utangamano wa kitaifa.
Askofu Mkuu Benson Bagonza |
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza ameliambia Raia Mwema kwamba hali ikiendelea na kuonekana ya kuwa ndiyo maisha ya kila siku, “kinachofuata ni machafuko kama haya yanayoendelea na kushuhudiwa.”
Katika mahojiano hayo maalumu, Askofu Bagonza alisema kwa sasa uongozi wa dola umeshindwa kujitofautisha na uongozi wa kisiasa na sasa viongozi wa dola wamekuwa wanasiasa......bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment