Thursday, October 30, 2008

Kashfa ya EPA:

Warioba, Lipumba

waijia juu serikali



Na Peter Edson na Noya Kizito

WAZIRI Mkuu wa zamani, Joseph Warioba amesema anashangazwa na kitendo cha serikali kufanya mazungumzo na wezi fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) badala ya kuwafikisha mahakamani akisema kufanya hivyo ni kuligawa taifa katika matabaka, ikiwa ni siku moja kabla ya muda wa mwisho waliopewa kurejesha fedha hizo.

Warioba, ambaye amekuwa akikemea rushwa, ukosefu wa uadilifu kwa viongozi wa umma na kuunga mkono harakati za kutetea wanyonge, alikuwa akizungumza kwenye kongamano la Haki za Binadamu lililomalizika jana jijini Dar es salaam.

Wakati Warioba akisema hayo, mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba pia alizungumzia suala hilo alipoitaka serikali kuwafikisha mahakamani wote waliochota fedha hizo, badala ya kuwasamehe wale watakaokuwa wamezirejesha kabla ya siku ya mwisho iliyowekwa na Rais Jakaya Kikwete ambayo ni kesho....bofya na endelea>>>>

No comments: