Tuesday, October 28, 2008



Mpe nyama ya ulimi uone!


Wiki iliyopita niliguswa sana na maoni yenu mliyoniandikia. Nataka nisema ahsante sana kwa wale wote mliotumia muda wenu kuniandikia na hata wale ambao mlishuka tu kumalizia kuisoma makala ile mpaka mwisho.

Lakini si hivyo tu, bali naomba pia nisema ahsante tena kwako kwa kuendelea kupitisha macho hapa na leo nakuja na maneno matamu ya kumpa mpenzi wako.

Wakale watakwambia "...Nenda kampe nyama ya ulimi mumeo utaona." Na kama utakumbua hata wiki iliyopita niligusia hili.

Sasa taratibu mwenzangu, usije ukakimbilia buchani, utachekwa; nyama ya ulimi kwa mwanamme ni yale maneno matamu anayopenda kuyasikia. Na ndiyo ambayo nataka nikuonyeshe leo nguvu ya maneno hayo.

Kule kwetu Tanga tunaambiwa si maneno tu kuwa matamu bali hata sauti ya manano hayo kwa mumeo shurti ivutie ati, ibadilishe kidogo iwe na deko deko. Ujue kubembeleza, uje kutumia maneno hayo matamu kumpumbaza mumeo, na ikibidi hata kupata unachotaka.

Wanawake wa mjini bwana huwa wanakosea hapo tu, na ndo' maana utasikia... "Loh mwanamke wa pwani akikuchukulia mume shoga sahau..." Kwani basi unadhani wanafanya mambo ya ajabu sana basi... Ni hiyo hiyo nyama ya ulimi ndio wanayotumia.

Maneno matamu kwa mumeo ni yale yanayotoka mdomoni kwa upole, kwa utaratibu yakiwa na ujumbe mzito wa kusifia, kutia moyo na kushukuru; hapo mwanamme umefikisha shosti......bofya na endelea>>>>>



No comments: