Rais wa Madagaska
awasili nchini
Rais Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais wa Visiwa vya Madagascar Marc Ravalomanana muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jumatatu kwa ziara ya kiserikali. (Picha na Mroki Mroki).
RAIS wa Madagascar, Marc Ravalomanana aliwasili nchini jana kwa ziara ya siku mbili kutokana na mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete. Ravalomanana aliwasili saa tisa alasiri jana akiambatana na mkewe na mawaziri watano na kupokewa na mwenyeji wake; Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein pamoja na baadhi ya mawaziri wa Tanzania.
Katika sherehe za kumpokea Rais huyo aliyewasili na ndege aina ya Boeing ya Serikali ya Madagascar, alipigiwa mizinga 12 na kukagua gwaride na kisha kuburudika na ngoma mbalimbali pamoja na matarumbeta yaliyotumbuizwa na kikundi cha Chama Cha Mapinduzi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ravalomanana atazungumza na Rais Kikwete na kwenda Zanzibar ambako pia atazungumza na Rais Amani Karume. Aidha, atapata nafasi ya kutembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro pamoja na Manyara.

No comments:
Post a Comment