Yaani wananchi
wanavyotupenda
wanatutupia mawe
Mpenzi Frank,
Unasemaje mpenzi, mboni ya jicho langu, faraja ya moyo wangu na tumaini la maisha yangu ya baadaye?
Nikikuwazia natabasamu,
Nikilala najazwa na hamu,
Na penzi lako tamutamu.
Kwa maneno mengine, nakumiccccc mpenzi, nakumic vibaya sana.
Lakini chunga sana na wewe maana za mwizi … mmnh sisemi. Mimi nilifikiri uongo wa siasa ni mambo ya jukwaani tu, kumbe…
Si juzi bosi alirudi na bonge ya ngeu! Jicho moja lilikuwa limevimba kiasi kwamba halionekani kabisa. Wacha Mama Bosi amkimbilie.
Kwa mara ya kwanza kwa miezi mitatu, yeye mwenyewe alimhangaikia, akahakikisha kwamba amekaa vizuri, akaleta ndala zake, akamletea hata na wiski yake huku bosi akilalama.
‘Jamani ee, siasa ngumu jamani. Yaani wananchi wanavyotupenda wanatutupia mawe.’
Wakati huu na Binti Bosi akaingia.
No comments:
Post a Comment