Saturday, October 25, 2008



Ansbert, Rais wa nchi

hapigwi mawe!


ANSBERT Ngurumo ni mmoja wa rafiki zangu wa siku nyingi na bado tu marafiki hadi hii leo. Tumefahamiana kupitia kalamu zetu. Siku moja kabla ya safari yake ya kwenda masomoni Hull, Uingereza nilikuwa nae. Siku hiyo   tuliagana kwa kunywa chai pamoja pale Namanga, Dar es Salaam.

Naweza kusema bila chembe ya shaka kuwa Ansbert Ngurumo ni mmoja wa waandishi mahiri waliopata kutokea katika nchi hii. Ansbert ana uwezo mkubwa, si tu wa kujenga hoja, bali pia kubomoa hoja za wengine kwa nguvu za hoja.

Ansbert Ngurumo ana nafasi kama kiongozi wa jamii kupitia maandiko yake. Ngurumo ana watu wengi sana wenye kufuatilia maandiko yake, mimi ni mmoja wa watu hao. Nafuatilia kwa makini kila kazi ya Ngurumo inayochapwa gazetini au kwenye mitandao......bofya na endelea>>>>>


No comments: