Monday, October 27, 2008

Young Africans (Yanga)

”Daima mbele,

nyuma mwiko”

yamaliza uteja

kwa Simba


Mchezaji wa Yanga Ben Mwalala akipachika bao wavuni huku kipa wa Simba Amani Simba akiuangalia bila bila kufanya lolote katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyia jana 
Dar es Salaam. YANGA 1, SIMBA 0.

...........................

UIMARA wa kipa Mzungu, Obren Curkovic, vurugu, imani za kishirikina na matukio yakiwamo ya mashabiki kurusha uwanjani chupa za maji ni baadhi ya matukio ambayo yalitawala mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyomaliza miaka karibu minane ya ubabe wa Simba dhidi ya Yanga.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa gumzo na ubishi mkubwa miongoni mwa mashabiki, Yanga imefaulu kushinda kwa bao 1-0 katika Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo uliokuwa wenye ushindani, ufundi mkubwa ikilinganishwa na mechi zinazohusisha timu hizo, Yanga walipata bao, dakika ya 15 kupitia kwa Ben Mwalala baada ya kupokea pasi ya Boniface Ambani ambaye aliwatoroka mabeki wa Simba.

Kabla ya ushindi wa leo, kwa mara ya mwisho Yanga kuifunga Simba katika Ligi Kuu, ni Agosti 5, mwaka 2000, kwa Yanga kushinda 2-0.

Sept 1, 2001, Simba 1, Yanga 0.

Agosti 18, 2002, Simba 1, Yanga 1.

Sept.  28, 2003 Simba 2, Yanga 2

Novemba 2, 2003 Simba 0, Yanga 0

Agosti 7, 2004 Simba 2, Yanga 1

Sept 18, 2004, Simba 1, Yanga 0

Aprili 17, 2005, Simba 2, Yanga 1

Agosti 21, 2005 Simba 2, Yanga 0

Oktoba 29, 2006 Simba 0, Yanga 0

Julai 8, 2007, Simba 5, Yanga 4

Oktoba 24, 2007, Yanga 0, Simba 1

Aprili 27, 2008 Yanga 0, Simba 0.


Yanga: Obren Curkovic, Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, George Owino, Godfrey Bonny, Shamte Ally, Athumani Iddy ‘Chuji’/Castory Mumbala, Benard Mwalala, Boniface Ambani/Amir Maftah na Mrisho Ngassa/Kiggy Makassy.

Simba: Amani Simba, Salum Kanoni, Juma Jabu, Kelvin Yondan, Meshack Abel, Henry Joseph, Nico Nyagawa/Mohamed Kijuso, Mohamed Banka, Emmanuel Gabriel/Ulimboka Mwakingwe, Mussa Hassan Mgossi, Haruna  Moshi. 




No comments: