Friday, November 28, 2008


Kwa nini wanashikilia

hadi wanabomoa

walichojenga wao?



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,

Vipi mwenzangu, mbona kimya hivyo?  Najua simu yangu ni kimeo ndani ya nchi kimeo lakini hata siku moja jamani umeshindwa kupenya?  Nami juzi nilijaribu kukupigia simu lakini wapi.  Kulikoni huko wewe uliye mbali na macho yangu lakini ndani ya moyo wangu?  Mimi mzima ila tu nakonda kwa kumkosa konda wa maisha yangu.

Hapa mambo yanaendelea kama kawaida, bosi mtetezi, MB mpatanishi, BB mchokozi.  Nadhani bila ugomvi kidogo wakati wa kula chakula chao hakitelemki.  Lakini wiki hii BB kawa mjanja kweli.  Akasifia kulia ili agonge kushoto.....bofya na endelea>>>>>


No comments: