Saturday, November 29, 2008



Tanzania na OIC:

Tuondoe utando,

tuangalie ukweli


Na Msiba Pakia 

Suala la Tanzania kutaka kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC) naona linatazamwa kwa mtizamo hasi tu na baadhi ya Watanzania na hivyo kulifanya lilete utata usio wa lazima. Mtizamo huu hasi unachochewa na ugonjwa tulioambukizwa na wakoloni wa gawanya utawale. Wakoloni walipandikiza makusudi saratani hiyo ili wajineemeshe kwa matatizo yetu. Tunakaribia sasa nusu karne tangu wakoloni waondoke lakini madhara ya saratani waliyotuachia yanaonekana mabichi. 

Kila nikiliangalia uwezekano wa Tanzania kujiunga na Jumuiya hiyo ya Kiislamu naona unakabiliwa na kigingi cha udini. Wasio Waislamu wanasema Tanzania inasilimishwa; hawataki kuangalia upande wa pili kama vile uwezekano wa kupata mikopo nafuu na misaada ya heri inayoweza kutuondolea ufukara na hivyo kuondokana na utegemezi. ...bofya na endelea>>>>>



No comments: