Thursday, November 20, 2008

Vunja mbavu


MTOTO KIKOJOZI


Mtoto mmoja alikuwa na tabia ya kukojoa kitandani kila siku na mama yake akaweka utaratibu kwamba kila akiamka kama mtoto huyo amekojoa anamchapa. 

Basi siku moja mtoto huyo alikojoa mpaka akaloanisha shuka lote. Mama alipoamka kama kawaida siku hiyo alimchapa sana hadi yule mtoto akawa ameumia matakoni.

Usiku yule mtoto ambaye hulala chumba kimoja na wazazi wake, akakosa usingizi kabisa ndipo alipomsikia mama yake akimwambia baba yake akojoe.

Mtoto kusikia vile akainuka na kusema, hata sikubali, mimi nikikojoa unanichapa lakini baba unamwambia aachie kojo. 

Duh! Mama kusikia vile alijisikia aibu na kuanzia siku hiyo mtoto akawa analala ‘sitting room’

Toka Global Publishers  (TZ)

No comments: