Thursday, November 20, 2008


Tunadai hatua

zichukuliwe wakati

wenye kuchukua hatua

ni sisi wenyewe



Kwa ndugu na majamaa,
Ushagoo,
Danganyika.


Mpenzi Frank,


Vipi mpenzi wangu?  Wajikunyata vipi na hali ya mvua?  Mimi mzima lakini wiki hii najisikia niko mbali zaidi na wewe maana mama bosi kanipeleka kwao, eti akienda huko wageni watakuwa wengi hivyo lazima nimsaidie mama yake katika kupika.  Kwa hiyo sasa mi mwenzio nina macho mekundu utadhani mchawi maana mama yake hataki kubadili maisha yake.

‘Sikiliza mwanangu. Nimepika humuhumu tangu niolewe.  Wewe umestawi na upishi wangu huohuo.  Mambo ya kusimama na umeme sitaki’

Na kweli anajua kupika.  Naona hutamtambua Hidaya wako kwa kunawili.  Napungua tu kwa kutafuta kuni asubuhiasubuhi.  Najua unafikiri nini, kwamba naweza kubebwa na kunawili kote huko lakini tunaenda kundi maana wageni wanaokuja kila siku si chini ya kumi. 

Kwa hiyo pole mwenzangu.  Najua wewe na wenzio mmekuwa walevi wa umbea wa wanene utadhani haya maigizo ya Wazungu kwenye luninga.  Lakini wiki hii ni mambo ya wembamba tu.  Sina habari bosi na wenzie wamefanya nini wala wamefanyiwa nini.  Badala yake michapo yangu yote ina harufu ya shamba, au kama wenzetu Wakenya wanavyosema, harufu ya ushagoo! ...bofya na endelea>>>>>


No comments: