ina maana gani?
Mpenzi Frank,
WAKUBWA Bwana. Kwa kuwa Krismasi imekaribia, nilijua angalau nitapewa ofu ya siku mbili tatu lakini nilipoongea na Mama Bosi akabaki anashangaashangaa.
‘Yaani wewe Hidaya una akili kweli? Wakati huu tunategemea wageni kibao wewe unataka kwenda likizo?’
Na kama kawaida yake alimaliza na kauli mbiu yake ya kila siku.
‘Kama umechoka kazi si useme tu! Wako wasichana wengi sana wanatamani kuwa na kazi hii.’
Iko siku mpenzi! Iko siku! Iko siku nitamwambia nimechoka nione kama hatajuta ninapoondoka na yeye akalazimika kumfunza mwingine. Si kwamba mimi ni mzuri sana lakini nimezoea kazi, nimezoea nyumba, najua natakiwa kufanya nini bila maelekezo. Lakini akija mwingine raha zote za MB zitaisha kwa angalau mwezi mmoja!....bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment