Monday, December 22, 2008

Watoto 9 kati ya 10

wa Kinorweji wana

Simu za mkononi






Takwimu zinaonyesha kuwa, watoto 9 kati ya 10 wa Kinorweji wana simu za mkononi (simkono)*. Wazazi wengi wanaamini kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuwa na mawasiliano na watoto wao, wakati wazazi wakiwa kazini au mbali na watoto wao. 

Kipindi cha kuanzia Desemba Mosi, hadi Desemba 23, kinaitwa "julestria" hapa Norway. Ni kipindi cha pilikapilika za matayarisho na manunuzi ya zawadi za Krismasi. 

Zawadi kubwa kwa watoto mwaka huu (inasadikiwa na watu wazima pia) ni simu za aina ya iPhone (picha hapo hapo juu). Hivyo wanatakwimu wanaamini kuwa idadi ya watoto watakaokuwa wanamiliki simu za mkononi (simkono) itaongezeka!!

* Mwandishi wa makala hii fupi amejaribu kufupisha "SIMU YA MKONONI" kuwa "SIMKONO" hiyo ni tafsiri yake mwenyewe. Sijui wapenzi wa Kiswahili, wataalamu wa Kiswahili, TUKI na BAKITA watauchukulia vipi ufupisho huo!!!

Makala hii imutumwa na Tausi Usi Ame Makame wa Oslo: tausi@online.no



No comments: