Thursday, December 25, 2008


Kama kila mtu anaona kinyesi

cha mwenzie bila kujua

anavyonuka yeye mwenyewe,

si mwisho tutakufa kwa harufu!


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Lo mpenzi wangu,

SIKU zinazidi kupita na jingo bezi zinazidi kila mahali lakini mimi nabaki nasikitika tu kwamba sitakula sikukuu hii na mpenzi wangu.  Jamani, kweli tutakuwa mbali hivyo?

Watu wote wanasherehekea, wanalishana mapochopocho, wanajisunda zao bichi, wanakumbatiana na wapenzi wao isipokuwa mimi tu.  Jamani nasononeka mpenzi, nasononeka sana! 

Lakini siwezi kukosa kukutakia heri ya sikukuu mpenzi wangu huku tukijiandaa kwa mwaka mwingine wa mapambano.  Iwe heri kwetu, tupate maendeleo, tuwe pamoja daima.  Au vipi mpenzi wangu?

Bofya na endelea>>>>>


No comments: