Watanzania hatusomi, hatudadisi
NILIPATA kusimulia kisa kifuatacho. Kuna wakati mwandishi wa safu moja ya gazeti nchini alipata kuambiwa na Profesa Seithy Chachage kuwa tatizo kubwa la wanafunzi wake, yaani wanafunzi wa Chachage, ni kutopenda kujisomea.
Jambo hili nilipata kuliandika huko nyuma. Lakini kwa vile bado ni tatizo kubwa, basi, tunahitaji kukumbushana. Chachage alisema wanafunzi hao wakiwa chuoni, husoma kwa ajili ya kufanya mitihani ili wavuke kwenda mwaka unaofuata. Kwamba mtindo wao wa kusoma ni wa madesa (vitini) tu na si vitabu.
Kwa mujibu wa mwandishi huyo, Chachage alilalamika kwamba wanafunzi walio wengi hushindwa kupambanua mambo kadhaa yanayowazunguka. Ni dhahiri, kwa anayefuatilia jamii yetu kwa sasa, hatapata taabu sana kukubaliana na maelezo ya Chachage kwa rafiki yake huyo...bofya na endelea>>>
No comments:
Post a Comment