Umemnunia, umemnyima
Sina mashaka mtakuwa muwazima hapo mlipo, na kwamba mambo yanaendelea kama kawaida yake huko mtaani. Kifupi tu ni kwamba kila kitu kiko kwenye mstari.
Shosti wenu kama kawaida yangu niko hapa kuwapasha. Watoto wa mjini wenyewe wanakwambia mambo mwake! Si ndio hivyo jamani. Basi mkaribie tu katika kona yetu hii.
Labda niende moja kwa moja kwenye pointi; kumnunia kisha kumnyimba unyumba shosti wewe inakusaidiaje labda?
Leo nataka niliongelee hili suala, inapotokea tofauti wengi wetu hukimbilia kununa ikifuatwa na uamuzi wa kumnyima unyumba mumeo.
Tukiamini kwamba kwa kufanya hivi ni kuwakomoa kwa nia ya kuwaadhibu hawa kinababa. Sasa hapa shosti ndipo tatizo linapoanza kwa mana tofauti na matarajio yetu hii ni tiketi iliyogongwa stemp kabisaaaa, isemayo
'NENDA KAPATE HUDUMA HII NJE'
Wangapi wanachukua uamuzi huu..? ni wengi. Leo nataka niseme ukweli hapa.
1. Ujue unajikomoa wewe mwenyewe
Mwenaume bwana nikama mtoto mdogo. Hii mkae mkijua shostito, akikosa kula nyumbani ataingia chumba cha jirani na akikaribishwa atakula, si ananjaa bwana.
Mwenzangu na mimi ukiwa umekaa ukiamini kwamba unamuadhibu kumbe ndio unampa upenyo aachane na ubwabwa wa nyumbani akalie jirani. Akinogewa huko shughuli sasa ndio itaanza rasmi, huku wewe ukitafuta mganga aliyerogewa mumeo kumbe ulianza mwenyewe kuchonga tunguri.
Ikitokea tofauti badala ya kununa siku tatu mi nakushauri useme naye kama kweli unataka kudumu na huyu mtu. Kwa sababu utakuwa umenunia kitu kidogo kumbe unatoa mwanya wa mambo makubwa zaidi.
2. Unauonyesha udhaifu wako...
Kama ulikuwa huna habari shosti sasa kaa nikwambie, hakuna wakati ambao mwanamke wa nje anafanya mahaba kwa bidii kama pale anopong'amua kwamba penzi la mumeo linalega lega kwako wakati yeye hana mamlaka nalo.
Hapo sasa ndipo kama wewe ni mwanamke uliyemnyima mumeo unyumba kwa madai eti umemnunia utaonekana kama hujui mambo. Si umetoa mwenyewe nafasi mzee akajionee? Sasa akishaonja asali mtu kama huyu hakawii kuchonga mzinga, halafu utaanza kulalamika kwamba umedhulumiwa kumbe ulijidhulumu mwenyewe na hasira zako zisizokuwa na msingi.
Ndiyo maana mwanzoni kabisa nikakwambia kama kuna tatizo lizingumzeni liishe kuliko kuamua kumnunia kwa siku tele, kumbe huenda ni jambo la kumalizika.
3. Unatafuta maambukizi?
Kama ni livyo sema; kumnunia mumeo kiasi cha kumnyima unyumba ni kumruhusu atoke nje akatafute pa kujikimu. Unamaana gani unapomzuia kula nyumbani akale wapi, si nje? maana njaa iko palepale...! sasa kama umetoa hiyo nafasi kesho na kesho kutwa usije kupiga makelele oooh nimeambukizwa, kwani umetaka wewe mwenyewe kuletewa.
Maana kumwachia huru ni kama kumuambia "Nenda kafanye utakavyo". Nimekwambia tangu awali kwamba masuala ya mapenzi mwanaume hatofautiani sasa na mtoto mdogo aliyenyimwa ubwabwa na mama yake akaenda kuula kwa jirani.
Mwisho huu unabaki kuwa ushauri, maisha haya na system hii ya kununiana sijui kama tunajilinda kwa maana ya kujilinda. Jamani tuwe tunaangalia nini tunafanya kabala ya kufanya, mambo mengine ni kujipa adhabu sisi wenyewe na kutafuta matatizo makubwa zaidi.
Kwa leo mwenzenu naomba niishie hapa, mambo mengine mpaka wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment