KUACHA MATITI NJE NI
FASHENI AU UMALAYA?
Tabia ya baadhi ya wasichana warembo kuvaa nguo zinazoacha matiti yao wazi imekuwa ikiacha maswali mengi miongoni mwa watu huku baadhi wakiuliza kwamba, kufanya hivyo ni sehemu ya urembo, fasheni au umalaya?
Wakiongea na Amani katika nyakati tofauti, baadhi ya watu wameeleza kuwa, wamekuwa wakishangazwa na staili hiyo ya uvaaji ambayo kwa namna moja inakwenda kinyume na maadili ya kitanzania...
Walidai kuwa, kwa mila na desturi za kitanzania kuna sehemu za mwili za mwanamke ambazo hazitakiwi kuonekana mbele ya wanaume ikiwa ni kuanzia kwenye matiti hadi magoti lakini wanashanganzwa na baadhi ya wasichana ambao hawaijali miili yao na kutembea nusu uchi.
“Kwa kweli nashindwa kuelewa kwamba hawa wasichana wanaovaa mavazi haya yanayoacha wazi matiti yao ndio huko wanakoita kwenda na wakati au ni umalaya? Kwasababu unamkuta msichana anatembea huku matiti yake na mapaja vikiwa nje na wala haoni aibu! Huku si kuwatega wanaume? Hivi mwanamke kama huyu akibakwa atamlalamikia nani?” alisema Bi. Margret mkazi wa Kinondoni jijini Da es Salaam.
Aliongeza kuwa, licha ya kwamba baadhi yao wakivaa wanapendeza na kusifiwa lakini katika suala la uvaaji ni vyema kila mtu akawa makini kwani wakati mwingine staili ya uvaaji wa mtu inaweza kumtambulisha kuwa yeye ni nani katika jamii na ana tabia gani.
Naye Aziza Bashir wa Manzese alisema kuwa, kila mtu ana uhuru wa kuchagua avae nguo gani, wakati gani na akienda wapi lakini mavazi hayo yawe na uwezo wa kusitiri sehemu nyeti ambazo si vyema zikaonekana mbele ya watu.
“Unajua wengine ukiwaeleza juu ya hili wanaona kama unaingilia uhuru wao, lakini wanashindwa kujua kwamba maamuzi yao lazima yaangalie na maadili ya nchi, huwezi kutembea uchi tukakuacha tu eti kwasababu ni uamuzi wako, lazima tuseme ili ikiwezekana ubadilike,” alisema mama huyo ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi.
Kutoka Global Publishers TZ
No comments:
Post a Comment