Na Elvan Stambuli
Kufua ishu ya kumfanya ombaomba ‘Matonya’, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi amebanwa na serikali kwa kupewa siku saba ili athibitishe madai yake kuwa kuna waziri mmoja kijana wa serikali anayemuhujumu ili afilisiwe. Hayo yalisemwa jana (Ijumaa) na Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha alipokuwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania kupitia kituo chake cha luninga cha TBC1.
Masha alisema tuhuma alizozitoa Mengi kuwa kuna mpango wa kummaliza ili afilisike ni nzito na anawajibika kutoa maelezo serikalini ndani ya siku saba.
“Madai yake ni mazito lakini kwa sababu anasema ana ushahidi wa kuhujumiwa na waziri mmoja kijana, tutamuomba atupe ushahidi na leo (jana Ijumaa) namuandikia barua ili atuletee,” alisema Masha. Alipoulizwa ikiwa hataleta ushahidi huo ndani ya siku saba serikali itafanya nini, Waziri Masha alisema sheria itachukua mkondo wake.
“Asipoleta ushahidi wake ndani ya siku saba, serikali ina wanasheria wake, watapitia sheria zinasemaje ili ichukue mkondo wake, hawezi kutoa madai mazito hayo eti kwa vile ana vyombo vya habari, ni hatari,” alisema Waziri Masha....bofya na endelea>>>>>
No comments:
Post a Comment