na hofu ya wapiga
kura mamluki 2010
WAKATI maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2010 yakiwa yameanza zinasikika kelele za kudai kuwepo mpango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ya Muungano kuvuruga uchaguzi huo, hasa kisiwani Pemba.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amedai kuwa CCM ambayo huwa haipati zaidi ya asilimia 10 ya kura kisiwani Pemba na kushindwa kupata hata jimbo moja, imeamua kutumia majeshi ya Zanzibar na ya Muungano kupelekea wapiga kura mamluki ili ishinde angalau majimbo sita kati ya 19.
Idadi ya majimbo ya uchaguzi Pemba ambayo ni ngome ya chama cha CUF, imekuwa ikipunguzwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kila unapofanyika uchaguzi kwa kile kinachoelezwa kama kutafuta ufanisi.
Hali hii imekuwa ikilalamikiwa na CUF kama njama ya kukipunguzia nguvu visiwani na hajulikani kama majimbo yatapunguzwa tena ka mara ya tatu katika uchaguzi ujao ili upatikane huo ufanisi unaotafutwa na ZEC
No comments:
Post a Comment