Ahadi ni kama benki. Madeni
yakizidi, basi hatuna
imani nayo tena
Mpenzi Frank,
AFADHALI natuma barua hii kwa pepe maana kwa jinsi mafuta yalivyofutika, nina wasiwasi kama barua zinaweza kufika. Mimi sishangai kwamba hawa wenye mafuta tumboni na vituo vya mafuta wanaogopa maharamia maana Waswahili wa Pemba …
Hujambo lakini? Mambo vipi huko? Yule mdogo wako anaonaje shule yake? Mimi mzima lakini kazi zimezidi maana bosi anapata wageni kibao ambao wanatumia mafuta yao ya mwisho kuja kulalamika kuishiwa kwa mafuta. Wengine wanabembeleza hata kupewa mafuta ya serikali na bosi anapokataa, wanakasirika.
‘Unaona! Ndiyo maana hamjali matatizo yetu. Mnarandaranda na mashangingi yenu huku sisi tunateseka! Si ajabu mnafurahi tukikosa mafuta maana jam zitapungua!’
‘Siyo hivyo Bwana shemeji. Tunafanya juu chini kurudisha hali ya kawaida!’
‘Mngekuwa mnafanya juu chini mngeachana na sikukuu kushughulikia hayo.’
No comments:
Post a Comment