Monday, January 26, 2009




Eti..? Wanaume

hawapekuliwi...?


Sina budi kuwashukuru kwa dhati ndugu, jamaa, marafiki na wasomaji wangu kwa mchango wenu kwangu wa mawazo ushauri na pengine sala, maana bila ninyi nadhani kona hii ingekosa msisimko.

Naomba Mungu azidi kuwajaalia nguvu, maisha marefu na mafanikio kwa mwaka huu mpya. Mungu awajazie imani na azidi kuzijaza nyoyo zenu matumaini na upendo.

Jamani eeeh... Eti..! wanaume hawapekuliwi!?

Eti ukimchunguza samaki hutomla?

Vipi kama umemhisi visivyo, labda unamashaka naye, haeleweki kiaina, haikuingii akilini unahisi lazima anaweza kuwa anakwendea kinyume, na hujathibitisha unawasiwasi, Hivi kuna haja kweli ya kumpekua kupata ukweli?

Nini wasiwasi huenda unataka tu kuwa na uhakika kujua kuwa unapendwa na kama kweli uko peke yako hata kama hakuna dalili zozote za kukuonyesha kuwa kuna kitu hapo, bado mtu huyu inabidi umpekue?

Lengo hasa la kumpekuwa linakuwa nini?... na Je baada ya hapo unajiuliza kama uko tayari kwa mtokeo au laa! na kama hivyo nivyo nini kitafuata.

Wengi wanasema nia ni kutaka kuokoa lakini pia unaweza kuwa unabomoa wakati unadhani unajenga kwa maana ya kutafuta tatizo urekebishe.

Sasa lipi jema? ukae utulie ama...!?

Leo naomba niongee kama dada..! Kiukweli kabisa.

1.Mtafute mtu ubaya wakati mambo yamegeuka na sivinginevyo...!

Kwanza ya yote kuna vitu shostito vya kuangalia; huyu mtu anakuheshimu kiasi gani anakupenda kiasi gani na anakujali kiasi gani.

Katika hili ukweli ni kwamba kama kweli unapendwa na unajua unapendwa sasa hapo watafuta nini kama si shari.

Na kama mnapendana muda huo kwa amani bila shaka huenda mkawa mko katika mapenzi moto moto na hapa sidhani kama unahitaji kumpekua huyu mtu kujiumiza roho bure.

Katika mtazamo wa kiume wenyewe wanasema inawezekana kumpenda mke wangu lakini nikamtamani Heriet lakini hili halina maana kuwa ni Heriet nataka kuwa naye, bali mke wangu. Basi kama hivyo ndivyo usimtafute ubaya mwenzio wakati mambo yako shwari unaweza kujitia jakaya la moyo bure!

2. Usije ukaguka kuwa kero lakini...!

Okay jamani...! Sio kweli kuwa kumpekuwa ni kumdhibiti na si kweli kuwa wanaume hawapekuliwi, kwa kuwa japo wengine wanadai hawajali lakini najua japo kwa siri au kwa kujua au kutokujua wanapekua.

Hata hivyo nataka kusema tu kuwa unapochimbua mambo unaweza kuwa chanzo cha mambo kwa maana kuwa unaweza kuamsha vitu ambavyo vitapoteza amani ambayo huenda ipo na una enjoy na labda kwa kufanya hivyo ukamfanya huyu kiumbe afikirie vinginevyo...! unaweza ukamdaut kwa kitu ambacho hakipo akilini mwake.

na unaweza kumpa picha kuwa kuna hati hati ya amani kuvunjika baina yenu. Na unaweza pia kuwa uanmtuma. Unaweza kujenga kutoaminiana na mwanaume kujishtukia. Utaonekana kama mtu anayemnatafutia ubaya mtu!

3. Angalia pia kiherehere chako kisijekuharibia...!

Unapompekuwa bila shaka unatafuta makosa! tuseme ukweli; hilo si jambo baya kufanya kama tayari hisia zako na ishara fulani zimeashiria kuwa huyu mtu lazima anakuwa anakutenda au kama huonyeshwi unapendwa.

Na hakuna ubaya mtu kulinda chakwako na hii kiu ya kujua ukweli kila mtu anayo LAKINI; unaweza ukakuta kitu kumbe sivyo unavyodhania. Umepekuwa umekutana na kitu umekiamini sivyo kwa kiherehere chako cha kusaka mambo.

Huenda ukawa umekutana na kitu ambacho kinabaki kuwa hisia zako tu tofauti na mapokezi ya kitu chenyewe... sijui naeleweka. Mfano zipo meseji watu wanatumiana "Vipi Dear!" unakuja, na hii ikawa ni meseji ya kawaida kabisa kwa mtu na mfanyakazi mwenzake kazini lakini kwako ikawa na sura nyingine tofauti kabisa na makusudiao yenyewe. Unakutana na meseji kama hiyo unaweza usimuelewe kumbe hamna kitu.

Mwisho tu nikuachie mwenyewe na mizani yako.

Mpaka wiki ijayo si vibaya mkaniambia hili nyie mnalionaje.

asmahamakau@mwananchi.co.tz


No comments: