Monday, January 26, 2009


Mkapa ajuta kubinafsisha

rasilimali za taifa kwa wawekezaji

bila mpango.......



RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, amesema anajutia kitendo chake cha kuliingiza taifa katika ubinafsishaji wa rasilimali bila ya kujiandaa kikamilifu na mabadiliko hayo.

Mkapa alitoa majuto hayo katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) uliofanyika Zanzibar wiki iliyopita katika Hoteli ya Zamani Kempinski na kuhudhuriwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki.

Mbali ya Mbeki, viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale - Mwiru.

Mmoja ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo ambaye alizungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa sharti la kutokutajwa jina lake, alisema Mkapa alikiri kuwa sera ya ubinafsishaji haijamsaidia kwa kiwango kilichotarajiwa Mtanzania na badala yake wamegeuka wageni katika rasilimali zao.

Chanzo hicho kilidokeza kuwa Mkapa alibainisha kuwa kukubali kwake sera hiyo kulikuwa na lengo zuri la kuwafanya Watanzania waondokane na lindi la umaskini kupitia uwekezaji utakaofanywa katika rasilimali zao.

“Alituambia sera ya ubinafsishaji inamuumiza mno, kwani alipoikubali hakutarajia kama ingeweza kuwafanya wageni wawe na sauti katika rasilimali za taifa kuliko wazawa kama ilivyo sasa,” kilisema chanzo hicho....


.....bofya na endelea>>>>>



No comments: