Mtangazaji mwenye jina kubwa nchini, Maimartha Jesse, ameanika siri za usagaji pamoja na kuyataja makundi ya wanawake wanaojishughulisha na ‘kamchezo’ hako kachafu...
Maimartha anayepiga mzigo kwenye Televisheni ya Afrika Mashariki, EATV, aliliambia Risasi Jumamosi mapema wiki hii kuwa siku hizi vitendo vya usagaji vinafanyika bila kificho.Aliendelea kusema kuwa hata wanawake ‘wanaodili’ na ‘kamchezo’ hako kachafu, hawajifichi na kwamba wanapenda wajulikane ili iwe rahisi kunasa wapenzi.
“Ni mambo ya jiji, maendeleo yanakuja na mambo leo, kwani kuna siri siku hizi besti? Usagaji upo hadharani na wanaoufanya wanajulikana,” alisema Maimartha na kuongeza:“Tena wengine wanaheshimika sana, machoni huwezi kuwadhania, wengine wana waume zao lakini hawaridhiki, kwahiyo wanajichanganya na wanawake wenzao kufanya uchafu wao.”
Akiendelea zaidi, Maimartha alisema kuwa tabia ya usagaji inakuwa kutokana na matatizo mengi ambayo wanawake wanakutana nayo kutoka kwa wanaume pamoja na kasumba ya kupenda kuiga.Alisema, wapo pia wanawake ambao wanakumbana na misukosuko kwenye ndoa zao, kama vile kusalitiwa na waume zao au kutotoshelezwa kimapenzi na ‘mamista’ wao, hivyo kujiingiza kwenye vitendo vya usagaji kwa lengo la kupata faraja mbadala.“
Yote ni tisa lakini kumi ni kwamba wengi wao wanaingia kwa kushawishiwa na wenzao, mfano mwanamke msagaji anamuona mwenzake anavutiwa naye, kwahiyo anamtongoza.“Ukweli ni kuwa vinara wa usagaji wengi wao ni watu wenye hela, kwahiyo huwashawishi mabinti kwa kuwahonga pesa ili wakubali, yaani hutongoza kama wanaume!”
Alisema Maimartha a.k.a Mrs. P Diddy.Aidha, Maimartha alitaja makundi ya wanawake ambao ni vinara wa usagaji kuwa ni wafanyabiashara wa kike wenye pesa ‘chafu’, baadhi ya mamisi, wanamuziki, wanenguaji, watangazaji na sehemu ya tabaka la vigogo serikalini.Aliendelea kusema kuwa kundi lingine ni wake wa vigogo nchini ambao alidai kwamba hulazimika ‘kuzinajisi’ ndoa zao na kujiingiza kwenye usagaji kutokana na kukosa tulizo la kweli kutoka kwa ‘mamista’ wao.Maimartha, alipochomekewa swali la kizushi na mwandishi wetu kuwa naye ni sehemu ya mmomonyoko wa tabia za kisagaji kwakuwa duka lake la Manywele lililopo Kinondoni, Dar es Salaam linauza nyeti ambazo hutumika kwenye usagaji, alijibu:“
Aku! Hapo unaelekea kwingine, lakini ukweli ni huu kwamba vile vifaa wanavyotumia kwenye usagaji vinauzwa bei mbaya lakini vinagombaniwa usiombe.”Mtangazaji huyo, pia alipotakiwa kutaja majina ya wanawake ‘wanaodili’ na kazi hiyo, alikuwa ‘mdogo kama piritoni’.“Aa ah, hapo tunatafutana ubaya, unataka mimi ndiyo niwe na maadui kwa sababu ya kazi yenu ya udaku?” Alihoji Maimartha.
No comments:
Post a Comment