Kwa nini wanasiasa
wanaogopa hukumu
za wananchi wanataka
hukumu za mezani tu?
Mpenzi Frank,
Paukwa!
AMINI usiamini, nimekutana na Makengeza wako. Na nimekubali mia kwa mia kwamba ni chizi. Tena chizi kabisa. Yaani kazi yake kuongelea matako tu, tuzo la tako, posho ya tako, anataka nini na matako yake?
Tena unajua alikuja hapa juzi maana Bosi alikuwa na kasherehe ka Noeli na anapenda kuwaalika na waandishi kidogokidogo. Bila shaka anadhani kwamba mwandishi aliyeshiba chakula cha wanene hawezi kuwasema tena. Kama wapiga kura. Eti kwa kuwa wamemwagiwa pilao, basi lazima wawe upande wao.
Sasa kwanza jamaa akachelewa eti gari liliharibika toka asubuhi na kule kwa bosi mabasi shida tupu. Pili kaRav kake kachafu utadhani tembo anayeogelea matopeni. Unajua analiita nini gari lake? Eti Miss Bantu. Eti gari lake lililotangulia aliliita Changudoa kwa sababu lilipendeza sana, lilikuwa dogodogo na liliweza kushindana na mashangingi barabarani. Gari la sasa Miss Bantu kwa sababu lina matako makubwa! Unamwona jamaa alivyo tu! Matakomatako basi. Nadhani tusi la tako litamrudia.
No comments:
Post a Comment