Thursday, January 22, 2009


Najiuliza kama huyo Obama

angekuwa na Baraka (Barack)

ya kusoma hapa kwetu...




Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


MPENZI Frank,


Sikuelewi mpenzi.  Kwa nini unataka kunishakiashakia kila wakati.  Mimi naishi kwa ajili yako, napumua kwa ajili yako, akili yangu yote na moyo wangu wote viko kwako lakini wewe ukisikia umbea wa aina yoyote, tayari umerukia uamuzi. 

Vibaya hivyo mpenzi!!  Mbona mimi nakuamini, maana mapenzi ni kuaminiana.  Bila kuaminiana kila kitu kinageuzwa kesi.  Wamwangilia mtu, au watabasamu bila kijijua tayari mwenzio kesharuka kilomita tatu na kuamini yule ni mpenzi wako.

Kwa hiyo mpenzi, sijui umeambiwa maneno gani lakini nasema kwa moyo mkunjufu kabisa, maneno yale yote uliyoambiwa ni uongo mtupu.  Mimi wako, sina mwingine na nasikitika sana kwamba wewe una imani ndogo namna hiyo.

Haya, nimesema, tena nimesema kwa uchungu mkubwa kabisa maana mimi ni binadamu pia.  Unavyonituhumu hivi waniua kabisa.

Bofya na endelea>>>>>


No comments: