Oslo, vurugu tupu!
Jana jioni kulifanyika maandamano mengine ya kupinga mjini Oslo ya kuipinga Israel. Maandamano hayo yalianzia nje ya Wizara ya mambo ya nchi za nje na yaliishia kwenye ubalozi wa Israel uliopo Parkveien, Oslo. Kulikuwa na fujo na vurugu tupu. Polisi walipigana na waandamanaji, ambao wengi wao walikuwa vijana wenye umri mdogo. Waandamanaji walianza kutupa fataki na "Molotov Cocktail" kwa polisi na kwenye seng´enge za kwenye ubalozi wa Israel. Polisi nao walijibu kwa kutumia mabomu ya machozi, mbwa na magari ya medani za kivita. Oslo kwa siku mbili mbili mfululizo, imekuwa uwanja wa mapambano! Maduka mengi ya katikati ya Oslo, yameharibiwa!!
No comments:
Post a Comment