Maneno bila meno ni
sifuri kabisa
Mpenzi Frank,
Usende mbali nami
Mimi nakupenda
Usitoke mbali nami
Mimi nakupenda
Umejaza roho yangu
Japo mbali nami
Nakuwaza kila saa
Japo mbali nami
WASIKIA hayo mpenzi? Na wewe unasemaje, faraja ya moyo wangu? Mwaka huu mtumba unakuwaje kwako? Mimi mzima kama si wazimu kwa kukumic!
Lakini hawa wa wizi mtupu wakiruhusiwa kuendelea kutugonga hivi naona nitakumic daima dumu. Mimi nashindwa kuelewa serikali inafanya kazi kwa vipi.
Wanatangaza bei mpya ya mafuta. Jana, siku ambayo bei zinatakiwa kuanza, hakuna anayezifuata. Wizi mtupu!!! Wanaendelea kuuza kwa bei ya mara mbili ya Marekani waziwazi, bila uoga, bila kushtuka kabisa. Lakini hata wanene wa nchi hii wananunua mafuta katika vituo hivi. Au wao wana kituo chao cha wanene peke yao ndiyo maana hawajui? Lakini hata kama wana kituo chao, bado ndugu zao, marafiki zao, walevi wenzao, waumini wenzao bado wanalazimika kununua kwa bei mbaya hiyohiyo. Wanawezaje kusema kwamba hawana habari kuwa wanapuuzwa moja kwa moja?
No comments:
Post a Comment