Sunday, February 08, 2009

Afanya ngono na wanaume

200 aliofahamiana nao

kwenye intaneti



Louise Grant (pichani) toka Manchester, Uingereza amesema kuwa "kufanya ngono na wanaume anaofahamiana nao kwenye mitandao ni salama zaidi kuliko kufanya ngono na wanaume wa kukutana nao kwenye baa".

Louise Grant alitoboa siri hiyo wakati akihojiwa na gazeti la News Of the World la Uingereza. Amesema amekuwa akifanya ngono na wanaume tofauti wastani wa kila baada ya siku tano. Kuna wakati alifanya ngono salama na watatu kwa siku moja.

Louise mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni meneja wa baa alisema " Rafiki zangu wamekuwa wakitembea na wanaume wanaokutana nao baa na hiyo ni hatari kwa kuwa wanaume ninaotembea nao napata nafasi ya kuwaona kabla sijakutana nao".

"Siku zote huwa nasisitiza ngono salama na huwa nabeba kondomu na kama mwanaume atalalamika huwa sikutani nae" alisema Louise.

Louise alianza kutengeneza orodha ya wanaume aliofanya nao ngono nao baada ya kuachana na mchumba wake miaka mitatu iliyopita.

Mwanamme wa kwanza alikutana naye kwenye mtandao wa Facebook kabla ya kuibukia kuwa mwanachama wa mitandao ya ngono akiwahi kurudi nyumbani kila siku toka kazini kusoma baruapepe za wanaume waliovutika naye.

Mwaka jana watu milioni 5.6 waliingia kwenye mitandao zaidi ya milioni 13 kutafuta wapenzi na kuishia kwenye mapenzi ya usiku mmoja. 

Chanzo cha habari: News of the World



1 comment:

Anonymous said...

Haya WABONGO mambo hayo tena mzungu ndio anafanya hivyo kazi mnaijuwatena kwakuwa mzungu amefanya itakubalika hapa bongo pia tusubiri tu