Wednesday, February 18, 2009


Bi. Karita Bekkemellem

awafananisha wavaa

hijabu, na wanawake

waliokeketwa!!!


Bi. Karita Bekkemellem


Malumbano ya matumizi ya hijabu/ushungi yamepamba moto na kuingia sura nyingine, baada ya Bi. Karita Bekkemellem  (Mbunge wa Arbeiderpartiet) kuwafananisha wanaotumia hijabu/ushungi na wanawake waliokeketwa. Aliyasema hayo kwenye kipindi Studio 5 cha TV FEM jana jioni.

Bi. Bekkemellem amewakasirisha watu wengi hususan Waislamu wa Norway na wengine wanadai kuwa Bi. Bekkemellem anawachukia Waislamu bila sababu na kuwa labda ni yeye akili yake imekeketwa!

Bi. Bekkemellem anapinga wazo la waziri wa sheria na polisi, Bw. Knut Storberget la kutaka kuwaruhusu wanawake wenye kutumia hijabu kuruhusiwa kutumia vazi hilo kwenye jeshi la polisi. Mwanzoni, Bw. Storberget alionyesha wazo chanya kutaka kukubali kuruhusu hijabu kwenye jeshi la polisi, lakini baada ya hilo kupingwa vikali na asilimia kubwa ya wanasiasa na wananchi wa Norway, Storberget ameingiwa na woga na kusema kuwa hilo la kuruhusiwa wanawake kutumia hijabu kwenye jeshi la polisi liangaliwe upya kwa mapana na marefu!



2 comments:

Anonymous said...

Huyu mama ana matatizo flani hivi. Ndio maana Jens Stoltenberg (Waziri Mkuu wa Norway) alimwondoa uwaziri! Alipokuwa waziri lake kubwa lilikuwa la wanawake wanaokeketwa kana kwamba lilikuwa jipya hapa Norway. Alikuwa hajui kuwa Chiku Ali (Mtanzania Mnorweji anayeishi Bergen, Norway) alilivalia njuga hili suala miaka mingi iliyopita kabla hata Wasomali hawajaanza kuingia kwa wingi hapa Norway!!!

Anonymous said...

Hili la kuvaa au kutovaa hijabu kwenye jeshi la polisi limeonyesha sura halisi ya Wanorwejiani. Wanorwejiani ni waoga kwa kitu kipya na kigeni hasa chenye taratibu, mila na tamaduni toka nchi nyingine. Fikiria hata wanasiasa wa vyama ambavyo ungedhani vinatetea haki za wote bila kujali rangu na asili ya mtu, wamepinga vikali hili la uvaaji wa hijabu!!!!

AMA KWELI MTU KWAO, WAHENGA WALISEMA!!!