Thursday, February 19, 2009

Malumbano ya hijabu

hapa Norway:

 

Polisi wa kike nchini Pakistani

wakipenda wanaweza kuvaa,

lakini siyo lazima



Inaruhusiwa kuvaa hijabu/ushungi kwenye jeshi la polisi Pakistani. 
Hapa polisi wa kike nchini Pakistani wakiwa kwenye paredi ya 
sikukuu ya Eid, Desemba 2008. 
Picha na Associated Press.


Malumbano ya kama polisi wa kike Norway wanaweza kuruhusiwa kuvaa hijabu au la yakiendelea, gazeti la kila siku liitwalo VG linaandika leo kuwa polisi wa kike nchini Pakistani wanaweza kuvaa hijabu/ushungi kama wakipenda. Naibu kamanda wa polisi wa Islamabad, Bi. Halena Iqbal Saeed analiambia VG kuwa wengi wa mapolisi wa kike hupendelea kuvaa kofia za polisi badala ya ushungi. 

Hili la VG kuandika kuhusu polisi wa kike wa Pakistani, linatokana na watu wengi kufananisha hili la uvaaji wa ushungi kwenye jeshi la polisi na nchi zingine ikiwemo Uingereza. Nchini Uingereza, polisi wa kike wanaopenda kuvaa vazi hilo wameruhusiwa miaka 10 iliyopita na ni polisi wachache sana nchini Uingereza wanaopendelea kuvaa vazi hilo.


No comments: