Thursday, February 05, 2009

Bora kujali kabla ya ajali


VIPI huko mpenzi wangu?  Umekwisha kupata trekta badala ya ile warsha ya UKIMWI?  Lo, itakuwa safi sana kama warsha zote zinageuzwa trekta lakini sijui hawa wanaotoa pesa watakubali.  Na baada ya hapo, kila mtu atapewa mafuta ya trekta badala ya posho ya warsha?

Unaonaje tukianza na waheshimiwa huko Dodoma?  Wanapofika katika kikao cha Bunge, kila mmoja akabidhiwe trekta aiendeshe hadi jimboni mwake.

Hapana, mpenzi usione nimepata wazimu.  Haya yalikuwa mawazo ya jamaa mmoja aliyemtembelea Bosi na kumletea mikikimikiki ndani ya nyumba yake mwenyewe.  Hadi Bosi akakasirika kama kawaida.

‘Nashindwa kuwaelewa watu siku hizi.  Kila siku serikali tunajitahidi kuja na mipango mizuri kwa ajili ya wananchi lakini kazi yenu kubeza tu, kubeza tu....bofya na endelea>>>>>



No comments: