Hassy Kitine:
nchi sasa
yaongozwa
kienyeji
MKURUGENZI Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania Intelligence and Security Service = TISS), Dk. Hassy Kitine, amesema taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la uongozi, ambalo halijawahi kutokea katika historia ya nchi.
Kitine ambaye aliiongoza idara hiyo nyeti kwa karibu miaka 30 zama za Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili, alisema ukosefu huo wa uongozi umesababisha nchi iongozwe kienyeji.
Kachero huyo namba moja kwa miaka mingi, ambaye alilazimika kujiuzulu wadhifa wa uwaziri wa nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, mwishoni mwa miaka ya 1990 kutokana na kuhusishwa na kashfa ya mkewe kufuja fedha za umma kiasi cha shilingi milioni 40, alirejea kutoa kilio chake cha miaka mingi cha kuporomoka kwa maadili ya uongozi nchini.
Kitine ambaye aliwahi pia kuwa Mbunge wa Makete kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alitoa matamshi hayo mazito katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa vyombo kadhaa vya habari.
“Hali tuliyofikia si nzuri, tena niseme ni mbaya sana. Kuna kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya uongozi. Na hii nawaambia, nchi haijawahi kuwa katika hali mbaya huko nyuma kama ilivyo sasa. Kwa hali tuliyofikia, ni vigumu kurekebisha maadili ya uongozi.
“Tatizo kubwa ni viongozi kukosa integrity (uadilifu). Kwanza ni integrity ya viongozi wenyewe, pili ni commitment (wito), tatu ni nationalism (utaifa). Haya ndiyo yalikuwepo wakati wa Mwalimu,” alisema Dk. Kitine.
Akizungumza kwa kujiamini kama ilivyo kawaida yake, Kitine alisema viongozi wengi wa serikali wamepoteza sifa kuu tatu za uongozi ambazo ni kuwa na uadilifu, wito na kuweka mbele utaifa, sifa ambazo alisema ndizo zilikuwa nguzo ya uongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, chini ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
“That was possible (hilo liliwezekana) chini ya Mwalimu. Kama alikuwa akifanya kosa, basi kosa hilo lilikuwa likitokea tu wakati akifanya jambo kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania.
“Philosophy (falsafa) ya Mwalimu, ilikuwa kwanza Mungu, pili Tanzania, halafu yeye binafsi. Kila kiongozi anayetofautiana na Mwalimu tu hulifikisha taifa hili kubaya, if you differ with him, utaishia kubaya,” alisema Dk. Kitine akionyesha hali ya masikitiko.
Alisema uteuzi mbaya wa viongozi, hususan ule wa mawaziri, umechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa viongozi wasio waadilifu, wengi wao wakijihusisha na vitendo vya rushwa.
“Haiwezekani viongozi wakateuliwa kwa misingi ya mitandao …sijui, kwa msingi wa politics of division (siasa za makundi) ndani ya chama. Haiwezekani nchi ikaendeshwa kienyeji. Integrity should be number one (uadilifu unapaswa kuwa kitu cha kwanza kuzingatiwa).
“Mtu anajiuzulu, anafukuzwa uwaziri kwa sababu ya kashfa, kwa sababu ya kukosa maadili, halafu anabakia kuwa mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya chama, nini hii? Hii haifai. Waziri akikosa uadilifu anatakiwa aondolewe mara moja nyadhifa nyingine zote alizobakiwa nazo. Nadhani hii itasaidia,” alisema Dk. Kitine pasipo kutaja jina la kiongozi yeyote.
Kitine ambaye wakati wote wa mazungumzo yake alisema alikuwa anataka kujadili masuala muhimu na si watu, alieleza namna asivyo na imani na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tatizo la rushwa kubwa.
Kwa mujibu wa kachero, mwanasiasa na mwanazuoni huyo, hatua hizo ambazo zinahusisha baadhi ya watu wenye majina makubwa kufikishwa mahakamani, zimechukuliwa kwa ajili tu ya maandalizi ya uchaguzi ujao.
“Nilikuwa kiongozi wa kwanza kuzungumzia rushwa kubwa miaka 10 iliyopita. Nilisema ndiyo inayovuruga uchumi kuliko hata rushwa ya nesi, hakimu, polisi,.… hakuna hata mkubwa mmoja aliyekamatwa. Ilinigharimu sana, na mimi nilipata adhabu ya kuzuiliwa kikao kwa miezi miwili, kama huyu nani huyu, Zitto (Kabwe). Wakati huo ilikuwa ndani ya CCM.
“Mimi nadhani hatua hizi zinazochukuliwa hazilengi kukomesha tatizo la rushwa, ni siasa tu za uchaguzi,” alisema Dk. Kitine.
Alipoulizwa nini kifanyike ili kukabiliana na tatizo hilo la uongozi mbaya, pamoja na mambo mengine, alielekeza changamoto zake kwa Idara ya Usalama wa Taifa.
“Usalama wa Taifa should be completely clean (unapaswa kuwa safi kabisa). Idara hii inatakiwa kuwa, juu ya mambo ya rushwa, iwe safi kabisa. Usalama wa Taifa ndiyo unayoteua viongozi, ndiyo inayoshirikiana na rais kwa kumshauri katika kuteua mawaziri. Sasa kama Usalama wa Taifa ukiwa mchafu ndio tunapata viongozi wala rushwa. Nafikiri vigezo vinavyotumika kuteua viongozi pia vina matatizo,” alisema Dk. Kitine.
Kada huyo wa CCM ambaye kitaaluma ni mchumi na mwanasheria, akizungumzia hali ya uchumi nchini, alisema kwa kiasi kikubwa uchumi umeshikiliwa na wageni kuliko wazawa, na kuelezea kusikitishwa kwake juu ya kuwepo kwa pengo kubwa kati ya matajiri na maskini.
Akitoa mfano alisema, miongoni mwa mambo yanayoonyesha kuparaganyika kwa mambo ni kukithiri kwa idadi ya ombaomba mitaani.
“Mwalimu asingeruhusu watu hawa waombeombe barabarani. Kazi za Watanzania ni udereva teksi, daladala, mabasi, kazi ya uboi ndani ya nyumba na kazi ya kufagia barabarani. Hizi ndizo kazi za Watanzania na hawa ndio wenye mali.
“Uchumi huu wa Watanzania si wa kwao. Watanzania ambao ni matajiri hawazidi hata watano. Hakuna sera bora za kusaidia kutumia maliasili zetu ili zitupe fedha ya kujenga shule, madaraja, hospitali…..” alisema Dk. Kitine.
Akizungumzia utendaji wa kazi wa Bunge katika kusimamia utendaji wa serikali, Kitine alisema kazi inayofanywa na taasisi hiyo hivi sasa ni kubwa kuliko ilivyopata kuwa wakati wowote huko nyuma.
Hata hivyo katika kuusifia utendaji wa kazi wa Bunge, aliupongeza mchango mkubwa na muhimu wa wabunge wa upinzani katika kuiimarisha taasisi hiyo muhimu.
“Ni Bunge zuri kuliko lilivyowahi kuwa huko nyuma. Linaonyesha kila dalili za uhuru. Upinzani unafanya kazi nzuri. Bunge liko wazi zaidi na wabunge wanatoa michango mingi yakinifu, yenye manufaa kwa taifa. Likiendelea hivi tutafika mahali pazuri,” alisema.
Toka gazet la Tanzania Daima mtandaoni.
Bofya na soma maoni ya wasomaji.
4 comments:
Kitine huenda alikula rushwa, lakini pamoja na hayo hapa ameongea. Naomba nichukue muda kidogo kutaja mambo ambayo yanaonyesha dhahiri kuwa maadili ya uongozi Tanzania yamezorota saana na nadhani CCM kama ilivyo kwa sasa haifai kuongoza Tanzania. Labda waondoke wote wale vigogo wabaki waadilifu wachache. Kwa sababu najua kuna waadilifu wachache CCM.
Napenda kwanza kutaja mambo ambayo yananishangaza. Naanza na recent incidences, Kwanza kama barua itanyofolewa kwenye faili katika wizara ya mambo ya ndani kama ilivyotokea kuondoka kwa barua kwenye issue ya vitambulisho na waziri mkuu ambaye ni kiongozi wa serekali akakiri hilo bungeni, je kuna usalama kweli? Mafaili ya wizara nyeti kama ya fedha yatakuwa salama?
Pili, ushahidi umetolewa wa kutosha kuhusu ufisadi wa watu kama Rostam, Kagoda na nakumbuka waziri mkuu alisema hadharani kuwa wamiliki wa kagoda hawako salama, lakini leo tunaambiwa ushahidi umepotea na tunaletewa kesi ya akina zombe ili vyombo vya habari vihamie huko tusahau, je kuna usalama hapo. Nataka sasa niamini kuwa fedha zilizoibwa kwenye akaunt ya EPA ni kweli ziliingingia kwenye kampeni ya Kikwete. Na kwa vile ni hivyo, hapo mpaka JK aondoke ndio tutajua ukweli, kama tunavyojua sasa kuhusu uongozi wa Mkapa. Serekali imeshindwa kabisa kupambana na ufisadi na nadhani kama wewe una nafasi ya kufanya ufisadi ufanye tu bora uhakikishe kuwa hukamatwi. Haiwezekani huyu jamaa anadaiwa bilioni 55 kama dhamana lakini anatoa milioni 880 na barua feki feki na anaachiwa wakati amefanya ufisadi wa nguvu. Ina maana, mahakama nayo ni corrupt, na kama mahakama ni corrupt unategemea nini?? Hapa naungana na Kitine kuwa nchi inaendeshwa kienyeji, na usalama wa watanzania uko mashakani. Huu ni uongozi wa ajabu kuliko uongozi tuliowahi kuwa nao tangia kuwa na taifa la Tanzania and i think we shall not have this kind of leadership. Akina Chenge wanacheka mtaani wakati watu wanakufa na njaa huko mtaani. Watu kama Liyumba wameiba wamewapa wanawake hela lakini kuna watu wanalala nja huko mtaani. Leo mnataka muwape watu wengine bilioni 200 bure kwa kuchapisha vitambulisho wakati wanafunzi wanagoma kupewa elfu tatu. This goverment has lost sight, bravo Kitine.
Kwanza, kigezo gani kilitumika kumpa uwaziri mtu kama Masha, au kwa vile ana umri mdogo na vijana walitajwa tajwa? Basi angechukua vijana makini, sio mtu kama Masha ambaye anaropoka ropoka. Jana anasema hakukutana na hii kampuni, leo anasema amekutana nayo. anasema kuwa hajaingilia mchakato lakini anakubali kuandika barua. Huyu hata hiyo sheria sijui kama amesoma au alipewa ya bure. Kuna mawaziri nadhani ni wachapakazi tu na hawakamatwi na kashfa za kishenzishenzi. Watu kama waziri wa miundombinu, ila na yeye amuondoe yule fisadi Mrema pale TANROAD.
Tatu, mauaji ya maalibino na bado siasa. Hivi kweli serekali with all its powers inahangaika na vita dhidi ya mauaji ya alibino?
Kikao cha mawaziri kinakaa leo bila hata kuwepo kwa media, lakini kesho yake unasoma kwenye vyombo vya habari waliyozungumza. Na aliyevujisha siri hajulikani, lakini ni ukweli mtupu wa hayo unayoyasoma. Sasa unashangaa, JK alichagua mawaziri au alichagua wambea. Wapo wapi kama akina Sokoine??
Namsifu kwa kusema ukweli na kwa uwazi na uzalendo, lakini kuna usahihi unahitajika kidogo:
1. Kitine hakumaliza Ph.D yake Canada, kwa hiyo si Dkt. kama anavyojiita. Muulizeni Profesa Luhanga wa Chuo Kikuu atawapa habari yote. Akikataa muulizeni Waziri Membe Bernard Membe au Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Sethi Kamuhanda.
2. Kitine hakuwahi kuongoza Usalama wa Taifa kwa miaka 30, haiingii akilini labda kama Tanzania ina miaka 100 na yeye ana miaka 150. Aliongoza kwa muda mfupi ambao haukufika hata miaka mitano. Muulizeni mwenyewe, akikataa basi muulizeni Joseph Butiku ambaye alikuwa Katibu wa Mwalimu, anawaju wakurugenzi wote wa enzi hizo.
Haya, salamu zao.
nimekaa kimya lakini naona nashindwa kuvumilia pamoja na kuwa si maadili kujibu hii kitu. Kwanza kabisa napenda kuwaweka wazi kuwa toka nchi hii ipate uhuru toka kwa mwingereza hakuna mkurugenzi wa usalama waTaifa alieongoza 30 years.
Pili huyo Hassy Kitine alishikilia kwa kipindi kifupi sana tena kipindi ambacho top alikuwa masomoni kidogo
(Lawrence Gama), mtu pekee alieongoza Idara hiyo kwa muda mrefu ni Colonel Apson Mwang'onda pekee.
Na hata huyo Mzena mnaemzungumzia hajawahi kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa! Yeye alikuwa Director tu wa Idara ya Ulinzi wa viongozi (Body Guard) sema tu aliacha historia wakati Jeshi lilipoasi yeye ndie aliemkimbiza Nyerere na kumficha Kigamboni kwa muda, na alipaswa kufanya hivyo kwa kuwa Idara yake inahusika na hilo moja kwa moja.
Kitine alikuwa mtumishi tu wa Usalama wa Taifa na alikuwa na cheo cha kawaida tu pale. Watu ambao wamewahi kuwa Wakurugenzi pale hadi sasa ni; Lawrence Gama, Wiliam Kussila, Lt. General Imran Kombe, Colonel Apson Mwang'onda, Balozi wetu wa kudumu UN Mr. Maiga, na kuna kipindi Simbeye aliwahi kukaimu kwa muda tu.
Ni Apson pekee ndie ameacha historia kubwa Usalama wa Taifa, siwezi taja amefanya nini maana maadili hayaruhusu kutoa mambo mengine gazetini.
Rashid Othuman ni mchapakazi mzuri sana, namfahamu pamoja na kuwa nilifanya nae kazi kipindi kifupi sana pale ubalozini kwetu London UK, na ana haki ya kumtumia Apson kwa kila kitu maana hamna mtu alieongoza Usalama wa Taifa kwa mafanikio kama Apson. Na ukizingatia Apson alimtumia vizuri sana R.O tokana na elimu yake na umakini ktk kazi.
Kama utahitaji kingine chochote kile kuhusu Idara hiyo niandikie mail natakueleza hadi jinsi team iliyotumwa kuugaraza upinzani na hadi leo wanasambaratika wao kwa wao.
Ni hayo tu
Kila awamu ya uongozi uliopita ilikuwa na Balance Sheet yake.Na utakapo ichambua kila Balance Sheet ya awamu fulani ya uongozi utangundua kwamba kila awamu ilikuwa na Assets na Liabilities katika Uongozi.Hakuna hata awamu moja itakayo diriki kutamka kwamba ilikuwa na NET ASSETS OVER POLITICAL LIABILITIES.Hakuna hata moja,hata ule wakati wa Nyerere,wakati wakina Kitine ndiyo waliokuwa Washauri Wakuu wa Sera na Dira ya Taifa.There were a lot of grave executive blunders in those times,so grave that it is not worth talking about them now!Hakuna Binadamu aliyekamilika,period!Na hizi Political Liabilities za kila awamu ya uongozi zilisukumiwa awamu nyingine na lawama zote kubebeshwa Kiongozi aliyefuatia.Rais anapochaguliwa na kuingia madarakani,muda mwingi sana,karibu nusu nzima ya kwanza ya uongozi wake ataitumia kushughulikia matatizo ya kiuongozi alaiyoyarithi kutoka uongozi uliopita.Na hivyo kumwacha na muda mchache sana wa kuonyesha makeke yake mwenyewe ya uongozi.Na asipokuwa mwangalifu katika kipindi chake chote cha uongozi atajikuta akizifanya kazi ambazo sio zake na hazikuwa katika Priority List yake ya Utendaji kama Rais.Hii ina maana gani katika mchakato huu tunao uzungumzia?Ni kwamba,mara zote atakayesikia maumivu ya Kiatu kilichobana ni yule aliyekivaa,na siyo mpita njia!Kila Rais wa nchi angependa kufanya makubwa sana pengine kuliko wenzake wote waliomtangulia.Kwanza,kwasababu hilo ndilo jukumu lake.Lakini kubwa zaidi,ni kwamba hakuna Rais aliyechaguliwa ambaye HAPENDI SIFA YA UTENDAJI BORA NA MAHIRI!Tatizo kubwa ninaloliona hapa kwetu,litahusiana sana na Mfumo wa Kiuongozi tuliourithi toka awamu ya kwanza,hatua kwa hatua hadi awamu ya sasa.Things have gone on for years unchallenged!As if everything was fine,absolutely fine.To put it more simply,ni kwamba katika kipindi chote cha Uongozi hapa nchini,nchi yetu imekuwa ikiongozwa kwanza na Mwalimu Nyerere,lakini wote waliofuatia ni wale waliokuwa Wanafunzi wa Mwalimu Nyerere.Kikwete pia alikuwa mwanafunzi wa Msekwa na wote walikuwa "under the influence of Nyerere's Doctrine/Philosophy!So,this country has never tasted any other leadership experience or leadership thought!We are still Zero Grazing in Political Leadership,to be Honest!Sio tatizo,but we need to be "Ourselves" not copycats!Hata nyumbani,malezi ya watoto usipokuwa mwangalifu kumpenda sana mtoto mmoja na kuwabagua wengine kunaweza kumharibu kabisa mtoto yule uliyempenda zaidi,na wale wenzie wakaja ongeza bidii zaidi na kumshinda yule uliyempenda mno.Tulaumu,lakini tuwe na mipaka.Umejengeka utaratibu hapa nchini,Rais akishashinda uchaguzi wale waliokuwa viongozi katika awamu zilizopita hawampi nafasi ya kupumua na uhuru wa kuamua mapya Rais mpya aliyeingia madarakani.Bali kila Kiongozi wa awamu iliyopita atamzonga Rais kwa njia yeyote ile ili ahakikishe na yeye atakuwemo katika Uongozi wake wa sasa!Hilo limekuwa likibeba Uchafu kutoka awamu zilizopita na kuuendeleza katika awamu zilizofuatia.We need to stop this Trend.Hii Global Economic Crisis ni Darasa muhimu sana kwa nchi maskini kama Tanzania kujifunza jinsi Uchumi wa Nchi utakavyo paswa kuendeshwa na kusimamiwa!This Global Economic Slump will be more beneficial to us,"Tanzania and the underdeveloped world",than to Developed INDUSTRIAL countries.This Economic Crisis has like it has opened-up the Pandora Box!The economic-growth magic formula has come out of the Pandora Box and now its up to those coutries with "Eyes and Brains" to see and reason!What to do Next!Nchi zina matatizo ya fedha na kiuchumi lakini bado tumeshika mabango kwenda kuomba omba Misaada,ni aibu ilioje!Kikwete may have his share of Blames to ponder,but more importantly,he is still too much you to afford Dogmatic and Utopian Thinking or Decadent Ideology which has been tested a Failure in the practical Past!Will Kikwete ever listen to this "Free Advice" he can not get from any University in this Planet?-----papperazzi antonnio----
Post a Comment