Kwa nini wakubwa hawawezi
kuona watoto wana akili zao,
na siri ya mtungi aijua kata
Mpenzi Frank,
Lo mpenzi wangu, najisikia mbali kwelikweli nawe maana wiki hii Mama Bosi ameamua kwenda kwao kwenye harusi ya mtoto wa binamu yake shemeji wa Bosi mwenyewe. Au tuseme hakuamua mwenyewe lakini bosi ameshashtukia mambo ya mwaka kesho kwa hiyo suala lolote lile linaloweza kumfanya apendwe na wananchi wa jimbo lake ni muhimu kwake.
Na kwa kuwa MB amelazimika kwenda, basi na mimi nimo maana MB hajaenda popote pale bila kuwa na mtu wa kumfulia nguo, na kusafisha viatu vyake hasa kama amepita kwenye matope ya nyumbani. Tena anachekesha mara nyingine anapojaribu kuvaa viatu virefu kwenye matope. Anayumba kama mlevi. Lakini ole wako akikuona unatabasamu kidogo maana atakushushia gunia la matusi!
1 comment:
Huyu mtunzi wa hizi barua za dada Hidaya mzuri na mahiri kweli. Angezikusanya na kuziweka kwenye kitabu hizi barua....
Post a Comment